Thursday, April 24, 2014

Watu 4 wauawa katika mlipuko Nairobi

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.

Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.

Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."
Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

BBC

No comments:

Post a Comment

Mkereketwa. Powered by Blogger.

Health

Documentary

News

Sports

» » » Watu 4 wauawa katika mlipuko Nairobi

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.

Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.

Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."
Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

BBC

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

About the Author Mwananchi Kweli

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

Video

Gossip

Movie

Technology

Photos