Friday, May 2, 2014

Amazon kutoa smartphone mpya kuwa mshindani wa Iphone,Nexus na Samsung.

Kampuni ya amazon inategemea kuzindua Simu zake za Smartphone ambazo zitatumia jina la Amazon na pia inasemekana kuwa na muundo wa Iphone5. Msemaji wa mtandao wa Amazon amesema kuwa wanategemea kuizidua september na itakuwa inauzwa kupitia mtandao huo wa Amazone ''Simu itakuwa na muonekano wa Iphone pia kama Google Nexus'' Alisema  BGR.

Inasemekana itakuwa na kioo chenye  ukubwa wa 4.7-inch ambacho kitakuwa na uwezo wa 720p HD Pia ram ni 2GB Processors quad-core Qualcomm Snapdragon.

The Amazon handset has a beveled edge similar to apple's iPhone 5

Apple's patented system is slightly different to the 3D display Amazon is rumoured to be working on. The first pictures of Amazon's 3D handset were revealed last week, pictured, and appeared to feature four cameras and retina-tracking technology that are used to create a 'floating screen' effect

The move would pit Amazon in a battle with Google and Apple, which is expected to unveil its latest iPhone in September

The handset is shown in a special protective case to shield its final design. However, the four cameras are clearly visible in each corner

he world’s first clear look at Amazon’s smartphone

TFF yachunguza usajili wa Domayo

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka (TFF) limedai linachunguza kitendo cha klabu ya Azam FC kumsajili kiungo Frank Domayo wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa mjini Mbeya.
TFF imedai imemuagiza Wakili Wilson Ogunde kuchunguza tukio hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa kambi ya timu ya taifa ina miiko yake.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa shirikisho hilo linampa siku 14 wakili Ogunde awe ameshachunguza tukio hilo na kuwapa ushauri wa kisheria na hatua za kufuata.
“Wakili Ogunde ataangalia mlolongo mzima wa tukio na kanuni za maadili kuhusu suala hilo, kanuni za usajili zinasemaje na tutafanyia kazi bila kumuogopa mtu wala kumuonea mtu kwa kumchukulia hatua stahiki.
“Hakuna ‘Mungu Mtu’ kwenye mpira wala klabu, yeyote aliyehusika na tukio lile tutamchukulia hatua za kinidhamu. Kambi ya timu ya taifa inatakiwa iheshimiwe, ina miiko yake na wahusika wote waliohusika kwenye tukio hilo tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria na ushauri utakaotolewa na wakili tuliyempa jukumu hilo, ndani ya siku 14 mtajua ni hatua gani tutazichukua,” alisisitiza.
Kwa kawaida, mchezaji anatakiwa achukuliwe hatua kwanza na uongozi wa timu na iwapo hautachukua hatua, basi suala lake linapelekwa kwenye kamati husika kwa hatua za kinidhamu.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, wakili wa TFF, Alex Mgongolwa alisema: “Kama Azam wamemsajili Domayo akiwa na mkataba na Yanga kama Domayo hana mkataba na Yanga, hakuna kesi, ila  kuna kingine cha maadili ambacho kinaweza kutengua usajili wa Azam kulingana na kanuni inavyoeleza.”

Operesheni ya kijeshi yaanza katika mji wa Slovyansk

Jeshi la Ukraine linaripotiwa kuanza operesheni ya kijeshi kuudhibiti mji wa Mashariki mwa Ukraine wa Slovyansk.Kuna taarifa kuwa helikopta moja imedunguliwa katika mji huo

Shirika la habari la Ujerumani Dpa limeripoti kuwa helikopta mbili za kijeshi zimedunguliwa na rubani mmoja ameuawa huku mwingine akitekwa nyara.Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine na kujiunga na Urusi wamesema wanajeshi hao wameanzisha kile walichokiita operesheni kubwa katika mji wa Slovyansk.Milio ya risasi na miripuko imesikika viungani mwa mji huo.Serikali ya Ukraine haijazungumzia operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza muda mfupi uliopita.Mengi zaidi kuhusu hali inavyojiri mashariki mwa Ukraine ni hivi punde.
Mwandishi:Caro Robi/dpa/Dw

Nguruwe wanaozurura kupigwa risasi India

Wanaharakati wamepinga vikali kuwaua Nguruwe wakisena ni kinyume na haki za wanyama
Maafisa wa mji wa Shivpur nchini India wamejikuta matatani kwa kuwataka watu wanaomiliki bunduki kuwapiga risasi Nguruwe wanaotembea ovyo mjini humo.
Wakazi waliamrishwa kubeba bunduki zao pamoja na leseni zao kuthibitisha wana idhini ya kumiliki bunduki ili kuweza kushiriki zoezi hilo. Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Hindustan Times.

Waliongeza kuwa wale watakaoruhusiwa kuwaua Nguruwe hao watateuliwa mwezi Mei.Maafisa wa utawala walisema kuwa wataweza kuwapa mikataba watu watakaoteuliwa kushiriki katika zoezi la kuwapiga risasi Nguruwe wanaorandaranda mjini humo, kulingana na malipo watakayotaka.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yamekasirishwa sana na pandekezo hilo la serikali.
‘‘Huu ni unyama na sio suluhu la tatizo la wanyama hao wanaorandaranda mjini,’’alisema Puneet Tripathi, mwasisi wa shirika la kutetea haki za wanyama na mazingira.
‘‘Lazima maafisa waangalie njia nyengine za kusuluhisha tatizo hilo labda kwa kuwahamisha wanyama hao hadi katika mji mwingine,’’ aliongeza bwana Puneet.
Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwapiga risasi Nguruwe itakuwa kinyume na sheria za India kuhusu ukatili.

Nguruwe wameonekana kama kero sio mjini humo pekee bali pia katika miji mingine nchini India. Huonekana mara kwa mara wakipekuwa kwenye majaa ya taka wakitafuta chakula.
BBC

Matunda na Mboga zinaokoa maisha

Watafiti nchini Uingereza wanasema kula matunda na mboga za majani mara saba kwa siku inakuwezesha kuwa na afya zaidi kuliko mara tano iliyokuwa imependekezwa hapo awali na shirika la afya duniani
Utafiti huu mpya unasema kuwa kula matunda mara saba kwa siku kunaweza kuokoa maisha yako kutokana na vifo vya mapema.

Eti wanasema kuwa ikiwa utakula matunda mara saba kwa wiki uwezo wako wa kupatwa na magonjwa yanayotishia maisha yako, unapungua kwa asilimia 42.Utafiti uliofanyiwa wanaume na wanawake, 65,226, ulionyesha kuwa matunda mengi aliyokula mtu mmoja yalimpunguzia uwezo wa kufariki katika umri wowote.

Wataalamu wanasema kuwa mifumo mingine ya maisha kama vile kutovuta sigara na kutokunywa pombe kupindukia pia imechangia kupungua kwa vifo.
Wanasema kuwa hawakuzingatia tu faida za Matunda na mboga bali mambo mengine mengi.
Watafiti katika Chuo kikuu cha University College London, walitathmini Data iliyokusanywa kati ya mwaka 2001 na 2008, iliyowapa mweleko kuhusu afya ya watu wanaokula matunda kwa wingi.
Utafiti huo ulitathmini idadi ya vifo kwa ujumla pamoja na vifo vinavyotokana na Saratani, maradhi ya Moyo na Kiharusi na kugundua kuwa vifo vya mapema vilipungua kulingana na mtu anavyokula matunda na mboga za majani.
Mboga za majani ndizo zilikuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi hjata zaidi ya matunda.
Maji ya matunda hayakuwa na manufaa makubwa huku matunda yanayopakiwa kwenye mikebe yakionekana kuongeza tisho la kifo.

Wataalamu wanasema kuwa wangali wanaendelea na utafiti wao na kwamba kuna mambo mengine mengi yanayochangia afya ya mtu.

ALIYEMTUPIA NDIZI ALVES AKAMATWA

Alves alikula Ndizi aliyotupiwa akisema vitendo vya kibaguzi vimekithiri katika soka Ulaya
Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya Jumapili akiwa uwanjani.
Dani ni raia wa Brazil anayesakatia soka yake katika klabu ya Barcelona.

Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati Alves alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili.
Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii.
Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Alves amesema kuwa amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi kwa miaka sita
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.
Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.
Barcelona walishinda Villareal mabao 3-2 katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa El Madrigal mjini Castellon pwani ya Hispania.
Alves aliambia BBC kuwa kilichomkumba sio jambo geni, na kwamba amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa miaka sita.

PHARRELL: ‘HAPPY’ HAIKUWA YANGU

Baada ya wiki kadhaa ya rekodi kuvunjwa na single yake ya ‘happy’ mwimbaji Pharrell Williams kwenye show ya Howard Stern ameeleza wazi kwamba single hiyo sio yake bali ni wimbo ambao uliandikwa na Cee-Lo Green na hakua anafahamu kuhusu wimbo huo mpaka pale Green alipoamua kumpa na kumruhusu aimbe.
Hii ni mara ya pili Williams anapata kitu kutoka kwa Cee-Lo sababu pia amechukua nafasi yake kama kocha mpya wa season ya saba kwenye mashindano ya kuimba ya The Voice.
Cee lo Green staa wa hit ya ‘forget you’
Kabla ya “Happy” Williams alikua ni Producer na mwimbaji ambae amewahi kuingia kwenye headlines za chati za muziki duniani kwa single kama kolabo na Snoop Dog na Jay Z na amewahi kuwaandikia nyimbo wakali kama Kanye West, Gwen Stefani, Gloria Estefan.

Pharrell pia aliwahi kumuandikia Michael Jackson enzi hizo lakini wawili hao hawakuweza kufanya kazi pamoja na nyimbo nyingi ziliishia kutumiwa na Justin Timberlake kwenye Album yake ya 2002 Justified.
Pamoja na kwamba Pharrell alimuandikia Michael Jackson hizo nyimbo hizo anasema timu yake ilizikataa, yani timu ya MJ ilizikataa hata baada ya Michael Jackson kuzipenda na kuzikubali nyimbo hizo baadae.
‘Nimefanya nyimbo nane kwa ajili ya Michael lakini zote hazikumfikia na ziliishia kurekodiwa na Justin Timberlake lakini baadae Michael mwenyewe aliniimbia hizo nyimbo na kusema zilitakiwa ziwe zake na nikamjibu kuwa zilikua za kwako’

Mkereketwa. Powered by Blogger.

Health

Documentary

News

Sports

Latest Posts

Video

Gossip

Movie

Technology

Photos