Monday, April 28, 2014

Vita kali kati ya waandishi wa habari wa Italia dhidi ya Super Mario Balotelli

Meneja wa klabu ya AC Milan Clarence Seedorf, amemkingia kifua mshambuliaji kutoka nchini Italia Mario Balotelli, kufuatia shutuma nzito zinazoelekezwa kwa mchezaji huyo kwa kigezo cha utovu wa nidhamu.
Clarence Seedorf, amemkingia kifua Balotelli wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sport Italia, ambapo amesema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kumzungumza vibaya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Seedorf amesema Balotelli amekua akibadilika siku hadi siku na tangu alipojiunga na AC Milan mwanzoni mwa mwaka huu, kama meneja amekuwa akiona mabadiliko hayo japo kumekuwa na mapungufu ya kibinaadam ambayo yanaweza kufanywa na yoyote yule.
“Nashangazwa na vyombo vya habari vinavyo muelelezea vibaya Balotelli, lakini kwa upande wangu sioni kama ana mapungufu kutokana na maelezo yanayotolewa dhidi yake.” Amesema Clarence Seedorf.
Vyombo vya habari vya nchini Italia vimekua vikimsema vibaya Mario Balotelli tangu mwishoni mwa juma lililopita kufuatia nidhamu mbaya aliyoionyesha wakati wa mchezo wa ligi ya nchini humo dhidi AS Roma ambao waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Suala kubwa ambalo liliwachukiza waandishi wa habari hadi kufikia hatua ya kumsema vibaya Balotelli, ni kitendo cha mshambuliaji huyo kutupa chini kinasa sauti (Microphone) wakati akihojiwa mara baada ya mchezo dhidi ya AS Roma kumalizika.
Balotelli akiwa katika mahojiano na waandishi wa habari hakuzungumza lolote licha ya kuulizwa swali ambalo lilihusiana na uwezo wake ambao haukuweza kuisaidia chochote AC Milan ambayo ilihitaji kushinda dhidi ya AS Roma kwa lengo la kujijhakikishia nafasi ya kusogea kwenye michuano ya Europa League.
Kutokana na uwezo dhaifu wa Mario Balotelli katika mchezo huo, meneja Clarence Seedorf alilazimika kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na   Giampaolo Pazzini katika dakika ya 69, hali ambayo ilimuongezea hasira mshambuliaji huyo.
Chuki za waandishi wa habari kwa Balotelli zimefikia hatua ya kumtaka kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli, kutomuita kwenye kikosi chake ambacho kitaelekea nchini Brazil kwenye fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment

Mkereketwa. Powered by Blogger.

Health

Documentary

News

Sports

» » » Vita kali kati ya waandishi wa habari wa Italia dhidi ya Super Mario Balotelli

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

About the Author Mwananchi Kweli

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

Video

Gossip

Movie

Technology

Photos