Wednesday, April 16, 2014

Mvua yailazimisha DAWASCO kuzima mitambo ya maji

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezima mitambo miwili ya uzalishaji maji kwenye mitambo yake ya Ruvu Juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani na Mtoni uliopo Temeke, Dar es Salaam.

Hatua ya DAWASCO imetokana na mvua kubwa zilizonyesha kusababisha madhara mbalimbali katika miji ya Kibaha, Pwani na Dar es Salaam.

Taarifa ya DAWASCO kwa vyombo vya habari jana ilisema sababu za kuzimwa kwa mitambo hiyo ni bomba la kupooza mtambo wa kuchota maji yanayotoka mtoni (cooling pipe) kuharibiwa na mafuriko namitambo ya kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji (Mto Kizinga) kuwepo ndani ya maji.

Taarifa hiyo ilieleza kutokana na sababu hizo maeneo yatakayokosa huduma ya maji ni Kijichi, Mbagala Zakheam, Mtoni kwa Azizi Ally, kwa Kabuma, Azimio Kaskazini na Kusini, Wailes, Mwembe-Yanga, Sudan, Mivinjeni na Mtoni Sabasaba. Maeneo mengine ni Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Chuo Kikuu, Kibangu, Riverside, Barabara ya Mandela, Tabata na Segerea.

“DAWASCO inawaomba wananchi radhi kwa usumbufu utakaojitokeza … kazi itaanza baada ya mafuriko kupungua Ruvu Darajani na Mto Kizinga,” ilieleza taarifa hiyo. ---
 Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

Mkereketwa. Powered by Blogger.

Health

Documentary

News

Sports

» » Mvua yailazimisha DAWASCO kuzima mitambo ya maji

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezima mitambo miwili ya uzalishaji maji kwenye mitambo yake ya Ruvu Juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani na Mtoni uliopo Temeke, Dar es Salaam.

Hatua ya DAWASCO imetokana na mvua kubwa zilizonyesha kusababisha madhara mbalimbali katika miji ya Kibaha, Pwani na Dar es Salaam.

Taarifa ya DAWASCO kwa vyombo vya habari jana ilisema sababu za kuzimwa kwa mitambo hiyo ni bomba la kupooza mtambo wa kuchota maji yanayotoka mtoni (cooling pipe) kuharibiwa na mafuriko namitambo ya kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji (Mto Kizinga) kuwepo ndani ya maji.

Taarifa hiyo ilieleza kutokana na sababu hizo maeneo yatakayokosa huduma ya maji ni Kijichi, Mbagala Zakheam, Mtoni kwa Azizi Ally, kwa Kabuma, Azimio Kaskazini na Kusini, Wailes, Mwembe-Yanga, Sudan, Mivinjeni na Mtoni Sabasaba. Maeneo mengine ni Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Chuo Kikuu, Kibangu, Riverside, Barabara ya Mandela, Tabata na Segerea.

“DAWASCO inawaomba wananchi radhi kwa usumbufu utakaojitokeza … kazi itaanza baada ya mafuriko kupungua Ruvu Darajani na Mto Kizinga,” ilieleza taarifa hiyo. ---
 Tanzania Daima

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

About the Author Mwananchi Kweli

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

No comments

Leave a Reply

Video

Gossip

Movie

Technology

Photos